Rais wa shirikisho la kimataifa la Mpira wa Miguu ( FIFA ) , Gianni Infantino ameipongeza timu ya Simba SC kwa kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ( VPL ) Msimi wa 2020/2021.

Katika barua yake kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Mguu Tanzania ( TFF ) , Wallace Karia, Rais wa FIFA Infantino alisema ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.
“Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC, Na kuwatia moyo waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano, Ari na Ushupavu, Alisema Rais Infantino katika barua yake.”
Pia alimshukuru Rais Karia na TFF kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa mpira wa miguu katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



Sarah
Asante kwa taarifa