Arsenal Yaichabanga Leicester Sebuleni Kwao

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuicharaza klabu ya Leicester City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani King Power kwa jumla ya mabao mawili kwa bila baada ya mchezo kuonekana kua mgumu kwa muda mrefu lakini vijana wa Mikel Arteta walifanikiwa kuondoka na alama zote tatu.

Mchezo huo uliopigwa mapema leo ulikua muhimu kwa timu zote mbili ambapo Arsenal walihitaji alama tatu ili kuendelea kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa, Huku Leicester nao wakihitaji kupata alama ili kuhakikisha wanajinusuru kushuka daraja msimu huu kama ambayo yaliwatokea misimu miwili iliyopita.mikel merino

Mchezo ulikua mgumu kwani kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya bila kufungana licha ya kua vijana wa Mikel Arteta walimilika mpira kwa muda mrefu wa mchezo, Huku vijana wa Ruud Van Nistelrooy nao walikua wakifanya mashambulizi ya kushtukiza mara kwa mara ambayo nayo pia hayakuzaa matunda na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Arsenal kuonekana kua na njaa ya kupata goli la haraka kutokana na namna walikua wanafanya mashambulizi langoni mwa Leicester, Lakini Mikel Merino dakika ya 81 na 87 alifanikiwa kuwapatia washika mitutu wa London magoli mawili ambayo yamewafanya kushinda mchezo huu ndani ya dakika sita.

Baada ya Arsenal kushinda leo sasa wanafanikiwa kufikisha alama 53 wakiwa nyuma kwa alama nne kwa vinara Liverpool wenye alama 57 hivo vijana hao wa kocha Mikel Arteta wanaendelea kuweka matumaini ya ubingwa hai, Kwani bado michezo imebaki mingi kwenye ligi hiyo kama wataendelea kupata alama tatu kwenye michezo yao wanaweza kufuta ukame wa  miaka 20 waliokua nao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.