Kiungo wa zamani wa vilabu vya Liverpool, Real Madrid, na Bayern Munich kwasasa kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen Xabi Alonso amefanikiwa kuongeza mkataba na timu hiyo mpaka mwaka 2026.

Xabi Alonso alijiunga na klabu hiyo mwaka mwezi Januari na kusaini mkataba mfupi lakini Bayern Leverkusen wamevutiwa na uwezo wa kocha huyo na kuamua kumuongezea mkataba mpya kocha huyo.Xabi alonsoBayern Leverkusen haikua kwenye kiwango bora sana wakati kocha Alonso anaichukua mwezi Januari, Lakini baada ya kuichukua klabu hiyo alionesha mabadiliko makubwa pamoja na kuipelekea nusu fainali ya michuano ya Uefa Europa League.

Kocha huyo amekua akihusishwa pia kuifundisha klabu yake ya zamani ya Real Madrid na kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti, Lakini haijakua sababu ya kumzuia yeye kusaini mkataba mpya na Leverkusen.Xabi alonsoKocha Xabi Alonso anatabiriwa kuja kua moja ya makocha bora sana siku za usoni na hiyo ni kutokana na ambacho anakionesha sasa, Vilevile kupitia mafunzo ya makocha kadhaa wakubwa kama Rafael Benitez, Jose Mourinho, Pep Guardiola pamoja na Carlo Ancelotti.


 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa