Chelsea wanaripotiwa kuwa mawindoni kumtafuta mrithi wa Eden Hazard klabuni hapo baada ya hatma ya staa huyo kutofahamika mpaka sasa. Hazard anatarajiwa kusepa Stamford Bridge na staa wa Barcelona anatarajiwa kuwa mbadala wake.
Nyota wa Barcelona ambaye pia alishawahi kuchezea Ligi Kuu ya Uingereza, Philippe Countinho amewekwa kwenye orodha ya wanaofaa kuchukua namba ya Hazard.
Hazard mwenye miaka 28 anaweza kumaliza tetesi za mda mrefu zinazomtaja kuwa atajiunga na klabu ya Real Madrid kwa kukamilisha uhamisho huo mwisho wa msimu huu. Countinho aliwahi kuchezea klabu ya Liverpool na anaweza kurejea tena.
Kama Barcelona watazingua kukubaliana na Chelsea, mshambuliaji wa Lille Nicholas Pepe anatajwa kuwa anaweza kuwa mbadala kwa Maurizio Sarri. Pele amekuwa akizivutia klabu kubwa za Ulaya baada ya kuchapa magoli 20 na kutoa pasi za magoli 12 kwa michuano yote.


Ester jackson
Habari nzuri hizi toa kitu weka kitu