Chiellini Amewajua Wabaya Wao

Klabu ya Juventus imeanza kampeni zake za kunyanyua vikombe vizuri baada ya kuwaburuza wapinzani wenzao wa jiji hilo AC Milan kwa goli pekee la mtu mwenye historia zake duniani kwa sasa Cristiano Ronaldo lililowafanya wao kunyanyua kikombe cha mapema kabisa ndani ya ligi kubwa tano kubwa duniani.

Kupitia hilo, mlinzi hatari na mkongwe wa klabu hiyo haoni kama ndani ya michuano wanayoshiriki kwa sasa kuna mwingine anaweza kuwazuia wao kuendeleza kampeni zao zaidi ya klabu nne zinazoshiriki michuano mikubwa ya klabu bingwa barani Ulaya. Kwake haoni kama kuna adui mwingine zaidi ya hao.

Ikumbukwe klabu hiyo haina bahati sana ndani ya michuano hiyo miaka mingi kitu ambacho kinawapa wakati mgumu mara zote labda kwa sasa ujio wa mkongwe Ronaldo unaweza kuwaneemesha wakawa na mwanzo mzuri ndani ya michuano hiyo, baada ya miaka mingi ya ukame wa kunyanyua taji hilo.

Chellini amezitaja klabu hizo kuwa ni Barcelona, Manchester city, Bayern munich na mabingwa wa kampeni hizo za msimu uliopita Real madrid. Akisema sababu za kila mmoja wa wapinzani wake anaona kwamba upande wao upo vizuri sana; lakini wanaweza kupata upinzani kutoka pande hizo nne kuelekea kuutafuta ubingwa.

Akiwazungumzia Barcelona, anaona wana nafasi ya kufanya vizuri sana msimu huu kutokana na kuwa na kikosi kipana ambacho kina wachezaji wenye uzoefu mkubwa sana na michuano hiyo; pia kikosi hicho kimekaa pamoja kwa muda mrefu kitu ambacho kama mchezaji anatambua kwamba kina msaada sana ndani ya timu.

Kwao Man city hata msimu uliopita wakionesha nafasi yao kubwa ya kufabya vizuri japo walitolewa na Waingereza wenzao, Liverpool. Anawapa nafasi kubwa ya kuonesha makali yao ya mwaka jana ndani ya mashindani haya yajayo na kuwaona wakiwa kizingiti kikubwa zaidi kama watakutana nao katika hatua yoyote.

Bayern munich kwa muda mrefu wamepotea kwenye ramani ndani ya michuano hiyo lakini Chiellin anaamini klabu hiyo itarejea kwenye uimara wake na kuwa mwiba sana kwa wapinzani wake. Hii ni kutokana na uzoefu wao katika michuano hiyo inayokaribia kuanza kutimua vumbi hatua ya 16 bora.

Pia anawaona Real madrid wakirudi kwa kasi ndani ya michuano hiyo na kuleta upinzani mkubwa pamoja na kuwa na matokeo mabovu kwenye ligi yao.

Katika hatua ya 16 bora Juve wataanza kutafutana na Atletico Madrid ili kuianza safari hiyo ya mtoano ambayo kila mmoja hutumia uwanja wake wa nyumbani. Atletico hapewi nafasi ya kufanya makubwa sana ndani ya michuano hiyo kutokana na matokeo yake mbalimbali ya msimu huu, lakini anapewa nafasi ya kuonesha upinzani pia katika michuano hiyo.

3 Komentara

    Juve inatisha sana.

    Jibu

    Juventus wapo vzr sana

    Jibu

    Chiellin makini sana ameisaidia juve vilivyo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.