Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, amesema amehuzunishwa na kipigo cha mabao 2-1 walichopata dhidi ya Newcastle United Jumatano, ikiwa ni mara yake ya kwanza kupoteza tangu achukue jukumu la kuinoa timu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa St James’ Park, mshambuliaji William Osula aliyeingia akitokea benchi alifunga bao la ushindi kwa Newcastle licha ya timu hiyo kubaki na wachezaji 10 uwanjani, jambo lililodhoofisha matumaini ya United ya kufuzu michuano ya UEFA Champions League.

Carrick, ambaye ni kiungo wa zamani wa Manchester United, alichukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo mwezi Januari na kabla ya mchezo huo alikuwa ameiongoza katika mechi saba akishinda sita na kutoka sare moja. Pia aliwahi kuwa kocha wa muda wa timu hiyo mwaka 2021 bila kupoteza mechi.

Mchezo huo ulichukua sura ya kipekee baada ya Jacob Ramsey kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano. Baada ya tukio hilo, Anthony Gordon aliifungia Newcastle bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kabla ya Casemiro kusawazisha kwa upande wa Manchester United.

Hata hivyo, United walishindwa kutumia faida ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi kipindi cha pili, huku Osula akifunga bao la ushindi mwishoni mwa mchezo baada ya kupenya upande wa kulia na kupiga shuti kali lililompita kipa Senne Lammens.
Akizungumzia matokeo hayo, Carrick alisema timu yake haikucheza kwa kiwango walichotarajia na kuongeza kuwa wanahitaji kurejea kazini na kujipanga vizuri zaidi katika mechi zijazo. Alisisitiza kuwa licha ya kupoteza mchezo huo, bado wana nafasi nzuri katika msimamo wa Premier League na wanaamini wanaweza kurejea katika kiwango chao bora.


