Mchezaji wa zamani FC Barcelona Clement Lenglet amesema kuwa umuhimu wa Harry Kane kwa Tottenham ni muhimu sawa na athari aliyokuwa nayo Lionel Messi wakati akiwa mchezaji wa Barcelona.

 

Lenglet Amesema Kane Yuko Tottenham kama Messi Alivyo kwa Barcelona

Beki huyo wa Ufaransa Lenglet anafahamika vyema na Lionel Messi ambaye alicheza naye Camp Nou na pia dhidi ya nguli wa Argentina wakati alipokuwa Sevilla. Messi alikuwa mchezaji wa klabu moja hadi mwanzoni mwa msimu wa 2021-22 wakati hali mbaya ya kifedha ya Barca ilipomfanya kuondoka kwenda Paris Saint-Germain.

Mshambuliaji huyo nyota alikua mfungaji bora wa muda wote wa klabu na mshindi wa rekodi ya Ballon d’Or mara saba akiwa Barca, huku akihesabu mataji 10 ya LaLiga na medali nne za Ligi ya Mabingwa kati ya wingi wa tuzo za heshima alizoshinda Los Cules.

Wakati Kane bado hajashinda medali akiwa na Spurs Lenglet, ambaye alijiunga na Tottenham kutoka Barca kwa mkopo katika dirisha la uhamisho lililopita alizungumzia athari alizonazo kwa klabu.

Lenglet Amesema Kane Yuko Tottenham kama Messi Alivyo kwa Barcelona

Katika nukuu zilizoripotiwa na Daily Mail, Lenglet alisema: “Unapokaa kwa muda mrefu katika sehemu moja na ukapata mambo mengi mazuri na klabu inamaanisha kuwa unakuwa sehemu ya klabu hiyo”

Lenglet alisema kuwa kwake Messi siku zote ni mchezaji wa Barca, na kwa Harry Kane ni sawa na ni vigumu kufikiria kuwa mshambuliaji huyo kuchezea timnu nyingine. Tottenham ni klabu kubwa, Harry ni mchezaji mkubwa na ni sehemu kubwa ya Tottenham.

Hakuishia hapo ameongezea kwa kusema kuwa Kane ni mfano mzuri kwa wachezaji wenzake wote huku akieleza jinsi ilivyo kucheza dhidi ya Messi, Lenglet amesema kuwa “Unacheza na mchezaji bora zaidi Duniani kwa maoni yangu”.

Messi anakusaidia kuimarika kila siku alicheza naye akiwa Barca na dhidi yake kwa Sevilla ni bora akiwa naye, huku akianza mechi tatu pekee za primia ligi kwa Spurs msimu huu lakini alisema kuwa alihitaji mazungumzo mafupi na bosi Conte ili kumshawishi kuhamia London Kaskazini, ambapo bado anaendlea kuzoea mtindo mpya wa maisha.

Lenglet Amesema Kane Yuko Tottenham kama Messi Alivyo kwa Barcelona

Lenglet ameanza mechi tatu pekee za Premier League kwa Spurs msimu huu lakini alisema ilihitaji mazungumzo mafupi tu na bosi Antonio Conte ili kumshawishi kuhamia London Kaskazini, ambako bado anaendelea kuzoea mtindo mpya wa maisha.

Tottenham inashika nafasi ya tatu kwenye Ligi kuu ya Uingereza na leo hii watawakaribisha Newcastle United nyumbani kwao baada ya kurejea kwenye kichapo mechi iliyopita dhidi ya United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa