Mwisho wa juma lililo pita uongozi unaosimamia mpira wa miguu nchini Uingeleza umejadili wazo la kumalizia ligi kuu ya Uingeleza kwa mtindo wa kukusanya vilabu vyote katika kambi maalum (KARANTINI) kama inavyofanywa katika mashindano ya Kombe la Dunia. Kambi hizo zitakazo wekwa nnje ya mji na baadhi ya maeneo tengefu ya jiji la London Inaweza kuanza mwezi Juni na Julai ili kumalizia msimu wa mwaka 2019-2020

Mikataba minono ya kurusha matangazo na sababu nyingine za kiuchumi zimeleta msisimko mkubwa kwa vilabu kumalizia msimu, huku ikiaminika kua ligi kuu ya nchini humo ndio itakua onesho kuu katika vipindi vya televisheni. Imethibitika kua mpango huo utahusisha kurusha mubashara nichezo yote 92 iliyobaki kwa kila siku katika kipindi chote cha majira ya joto.
Ili kukamilisha mpango huo, vilabu na wafanya kazi wake wata tengwa kwenye hoteli zitakazo andaliwa na watawekwa mbali na familia zao kama ambavyo mashindano mengine ya kimataifa hufanyika. Wahusika watapimwa na kubaki kalantini kwa kipindi kitakacho kitakacho hainishwa, huku lengo likiwa ni kupunguza hatari ya kusambaa kwa virusi vya Corona (COVID19) kwa maana ikitokea moja ya watu watakao tengwa ata bainika kua na virusi hivyo atavuruga mpango huo.
Uongozi wa ligi kuu pia umejiandaa kutenga hospitali rasmi kwa ajili ya wachezaji watakao pata majeraha kipindi ambacho mashindano hayo yanaendelea. Viwanja vitakavyotumika pia ni vile vya mazoezi na vilivyo nnje ya miji huku kiwanja cha St George Park kiki husishwa na baadae kutolewa.

Tukuo kubwa kama la Ligi kuu ya nchini Uingeleza itachukua muda kidogo kurudi katika hali yake na kua sawa kama awali lakini kurudi kwake itakua chachu kwa viongozi selikari hususan kwenye nyanja za kiuchumi.
Hali ilivyo sasa ni kua kila kitu kipo mezani na kimeshajadiriwa, hili wazo la kutumia mufumo wa kombe la dunia kuendesha ligi kuu lilikuepo mwanzoni mwa mwezi machi , lakini vilabu havikuunga mkono ingawa kwa sasa ina himizwa zaidi.
Ni hakika kua hakuna timu itakayo ingia uwanjani bila kupitia vipimo na kujiridhisha.

