As Roma Dhidi ya Bayern Leverkusen ni Vita ya Mwalimu na Mwanafunzi

As Roma itashuka dimbani usiku wa leo wakiwa nyumbani katika dimba lao la Olympico kuwakaribisha Bayern Lverkusen ya nchini Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Europa ligi.

Mchezo wa leo kati ya As Roma na Bayern Leverkusen utakua wa kuvutia hisia za mashabiki wa mpira wa miguu, Kwani utakutanisha kati ya mwalimu na mwanafunzi wake ambapo Jose Mourinho ambaye anaifundisha Roma atakabiliana na mwanafunzi wake Xabi Alonso ambaye ni kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen.as romaJose Mourinho amewahi kufanya kazi na Xabi Alonso ndani ya klabu ya Real Madrid mwaka 2010 mpaka mwaka 2013 akiwa kama kocha wa klabu hiyo huku Alonso akiwa kama mchezaji ndani ya klabu hiyo, Hivo kutokana na uhusiano huo mchezo huo utakua wenye kuvuta hisia za mashabiki wa mpira wa miguu leo.

As Roma chini ya kocha Jose Mourinho imefanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya ulaya ambapo msimu uliomalizika kocha huyo aliiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa michuano ya Uefa Conference League, Mwaka huu wamefanikiwa vilevile kufika nusu fainali ya michuano ya Europa League kutokana na ubora ambao wameuonesha.as romaKlabu ya As Roma itakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Bayern Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso kwani kocha huyo kijana amefanikiw akuifanya timu hiyo kua bora tangu amekabidhiwa timu hiyo, Hivo mchezo wa leo unatarajiwa kua mkali na wenye ushindani mkubwa baina ya mwalimu dhidi ya mwanafunzi wake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.