Mkurugenzi wa Juventus, Giorgio Chiellini, hakutarajia Luciano Spalletti kuwa na athari ya haraka kiasi hicho, lakini akaeleza sababu ya kutosajiliwa kwa mshambuliaji mpya kuelekea robo fainali ya Coppa Italia dhidi ya Atalanta.

“Kwa kawaida timu zote mbili zinaujali sana mchezo huu, kwani ni robo fainali. Tunafahamu ugumu na kasi inayohitajika ili kuendana na Atalanta, lakini tutajitahidi kutoa kila kitu ili kushinda”. Chiellini aliiambia Sport Mediaset.
Kenan Yildiz hayuko fiti kwa asilimia 100 kutokana na tatizo la misuli huku Dusan Vlahovic na Arek Milik wakiwa majeruhi wa muda mrefu, hivyo Andrea Cambiaso amehamishwa kucheza nafasi ya juu zaidi upande wa kushoto.
Usajili wa siku ya mwisho Emil Holm na Jeremie Boga wamekaa benchi kwa mara ya kwanza, lakini mshambuliaji aliyesubiriwa kwa muda mrefu hakupatikana baada ya juhudi kushindikana za kuwasajili Randal Kolo Muani, Jean-Philippe Mateta na Youssef En-Nesyri.
“Nadhani tuliichunguza kwa kina soko la usajili na kuangalia hali mbalimbali ambazo zingeweza kutusaidia wakati wa kutokuwepo kwa Dusan Vlahovic,” Chiellini alieleza.
Chiellini alisema kuwa anatarajiwa kurejea hivi karibuni, lakini si mwezi huu, na kisha watahitaji kuona atachukua muda gani kurejea kwenye kiwango chake kamili baada ya jeraha la muda mrefu.
Wa meridhishwa na jinsi timu inavyoendelea kukua, kwani baadhi ya wachezaji wanaanza kujiamini zaidi. Pia wamefurahi kuona Federico Gatti akirejea na wanatarajia wengine pia kuongeza mchango wao, ili kusaidia timu katika kipindi kigumu lakini chenye msisimko.


