Fountain Gate FC Yahamia Arusha, Yaiaga Manyara

Klabu ya Fountain Gate FC imetangaza rasmi kuhamishia makao makuu ya shughuli zake Mkoa wa Arusha kuanzia leo Februari 06, 2026, ikiwa ni hatua mpya ya kimkakati kwa maendeleo ya timu hiyo ndani na nje ya uwanja.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo, Fountain Gate FC imetoa shukrani za dhati kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara, mashabiki, wadau pamoja na viongozi mbalimbali kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kipindi chote ambacho timu hiyo ilikuwa ikiendesha shughuli zake mkoani humo.

Fountain Gate FC Yahamia Arusha, Yaiaga Manyara

Uongozi umeeleza kuwa kipindi cha uwepo wao Manyara kiligubikwa na mafanikio na mshikamano mkubwa kutoka kwa jamii, jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa klabu hiyo kiushindani na kiutawala. Klabu imesisitiza kuwa ushirikiano walioupata utaendelea kubaki kuwa sehemu ya historia muhimu ya Fountain Gate FC.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi wa kuhamia Arusha umelenga kufungua fursa zaidi za kibiashara na kiuwekezaji, pamoja na kuboresha miundombinu na mazingira ya maendeleo ya timu kwa ujumla. Hata hivyo, klabu imefafanua kuwa Mkoa wa Manyara utaendelea kuwa nyumbani kwa Taasisi ya Fountain Gate, ambapo timu za vijana na wanawake zitaendelea kuendesha shughuli zao kama kawaida.

Mapokezi rasmi ya timu yatafanyika hii leo 06, 2026 katika Mkoa wa Arusha, kuanzia saa 5:00 asubuhi. Uongozi wa klabu umewakaribisha mashabiki na wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu katika historia ya klabu.

Fountain Gate FC Yahamia Arusha, Yaiaga Manyara

Fountain Gate FC imehitimisha kwa kuwashukuru tena wakazi wa Manyara kwa upendo, mshikamano na sapoti waliyoionesha, huku ikiomba ushirikiano kama huo kuendelea katika ukurasa huu mpya wa klabu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.