Lindelof Aingia Kwenye Rada za Inter Milan

Victor Lindelof ameingia kwenye rada za klabu ya Inter Milan wakihitaji kupata saini ya beki huyo wa kimataifa wa Sweeden ili kuziba pengo la beki wake Milan Skriniar ambaye atatimkia PSG mwishoni mwa msimu.

Klabu ya Inter Milan inawaza namna ambavyo itaweza kuziba pengo la Milan Skriniar ambaye amemalizana na klabu ya PSG, Hivo wababe hao wa soka nchini Italia wanafikiria kumsajili Victor Lindelof kama mbadala wa beki huyo ambaye alikua nguzo muhimu ndani ya timu hiyo.LindelofBeki huyo wa kimataifa wa Sweeden ni wazi anaweza akafikiria kuondoka ndani ya klabu ya Manchester United kwani amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara chini ya kocha Erik Ten Hag, Hivo kama Inter Milan watakua makini kwenye kuhitaji saini yake anaweza kujiunga nao.

Taarifa za ndani kutoka klabu ya Manchester United zinaeleza licha ya mchezaji huyo kutokua chaguo la kwanza ndani ya timu hiyo, Lakini klabu ya hiyo inataka kumbakiza nyota huyo ndani ya kikosi chao hivo hii inaweza kua changamoto kwa klabu ya Inter Milan.LindelofKlabu ya Inter Milan wameanza mipango hiyo mapema ya kutafuta mbadala wa kusajili mbadala wa Milan Skriniar ambaye ni wazi hatakua mchezaji wao kuanzia msimu ujao, Hivo wakifanikiwa kumalizana na beki huyo wa klabu ya Manchester United Victor Lindelof  mapema wanaweza kuepuka ushindani mkubwa katika dirisha kubwa.

Acha ujumbe