Rafael Leao anakiri kuwa si mchezaji aliyekamilika na hana chochote dhidi ya kocha wa Milan Paulo Fonseca, lakini bado hakubaliani na baadhi ya shutuma za maadili yake ya kazi.

Mshambuliaji huyo kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kimataifa na Ureno na kujiamini kwake kulichochewa sana na uchezaji wake kwenye Uwanja wa Estadio Bernabeu, ambapo Milan waliichapa Real Madrid 3-1 kwenye Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, bado alishutumiwa na mchambuzi wa Sky Sport Italia na beki wa zamani wa Rossoneri Alessandro ‘Billy’ Costacurta kwa kuweka tu juhudi wakati wa mechi kubwa na kuwa na maadili duni ya kazi, kumaanisha kwamba hakuwa katika wachezaji 100 bora duniani.
“Ni wazi sikubaliani na hilo. Nimekuwa na msimu mzuri huko Milan lakini, kama kila mtu mwingine, kuna kupanda na kushuka. Kampeni ndiyo kwanza imeanza. Angalia, najua kwamba mimi si mchezaji kamili na wakati mwingine naweza kufanya vizuri zaidi. Sitingishwi na ukosoaji huu, nina watu wanaonisaidia kuimarika na hao ndio natakiwa kuwasikiliza. Ukosoaji huu unanichochea kujibu uwanjani.” Alisema Leao.


