Wakati kukiwa na fukuto kwamba huenda Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga atakutana na mkono wa Thank You, kocha huyo bado yupoyupo kwa kuwa ameanza kuwanoa wachezaji wa timu hiyo kuelekea mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga imetinga hatua ya makundi ambapo inatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga hilo na itakuwa na kazi dhidi ya Al Hilal ya Sudan mchezo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 26 2024.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Tetesi zinaeleza kuwa Gamondi yupo kwenye hesabu za kusitishiwa mkataba wake wa mwaka mmoja aliongeza kutokana na mwendo wa timu hiyo kutokuwa bora ndani ya msimu wa 2024/25 ambapo timu hiyo imepoteza mechi mbili mfululizo.