Winga wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Ac Milan inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A Rafael Leao amejitia kitanzi ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2028.
Winga Rafael Leao amekua kwenye mazungumzo ya muda mrefu na wababe hao wa soka kutoka nchini Italia juu ya kuamua kuongeza mkataba mpya ndani ya timu hiyo, Hatimae jambo hilo limetimia na mchezaji huyo atapatikana ndani ya viunga vya San Siro mpaka mwaka 2028.Winga Rafael Leao amekua kwenye kiwango bora tangu ajiunge na klabu hiyo huku akifanikiwa kua mchezaji bora wa ligi ya Italia msimu wa 2021/22 kitu kilichomfanya thamani yake kupanda na timu mbalimbali kuanza kuvutiwa na mchezaji huyo, Hivo Ac Milan wakahitaji kumuongezea mkataba winga huyo ili kuepuka usumbufu wa vilabu vingine.
Rafael Leao amesaini mkataba mpya na Ac Milan ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2028, Lakini kuna kipengele kwenye mkataba wake kitakachomruhusu kuondoka ndani ya timu hiyo pale ambapo timu yeyote inayomtaka itafika dau la Euro milioni 175.