AC Milan Watulia Kuhusu Mustakabali wa Leao

Rais wa klabu ya AC Milan, Paolo Scaroni ametulia kuhusu mustakabali wa Rafael Leao huku kukiwa na mazungumzo juu ya mkataba mpya wa mshambuliaji  huyo anayewindwa na vilabu vingi.

 

AC Milan Watulia Kuhusu Mustakabali wa Leao

Leao amekuwa kificho kwa Rossoneri na alichangia pakubwa katika ushindi wao wa taji la Serie A msimu uliopita,huku mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ureno amekuwa akihusishwa na vilabu vya Real Madrid, Paris Saint-Germain na Liverpool.

Leao amepewa kandarasi na AC Milan hadi Juni 2024 na Scaroni ana matumaini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ataongeza muda wake wa kukaa San Siro. Rais huyo amesema kuwa ameambiwa kuwa mchezaji huyo anajisikia vizuri na kwamba ana motisha.

AC Milan Watulia Kuhusu Mustakabali wa Leao

Scaroni aliongeza kuwa; “Ninajua kwamba Mkurugenzi wa kiufundi wa Milan Paolo Maldini anajadiliana naye na nilivyosema tu kama atafanya mazungumzo, mimi ni mtulivu.”

Leao alifunga dhidi ya Ghana na Uswizi katika Kombe la Dunia kabla ya Ureno kubanduliwa nje na Morocco katika hatua ya robo fainali nchini Qatar.

Acha ujumbe