Inaripotiwa kuwa klabu ya AC Milan wameanza kuvutiwa na mchezaji wa Manchester City Jack Grealish huku mustakabali wa mchezaji huyo akiwa na miezi 18 katika klabu hiyo licha ya mkataba wa miaka sita.
Kiungo mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 hajatimiza matarajio yake tangu anunuliwa kwa pesa nyingi kutoka Aston Villa akiwa ni nyota wa klabu hiyo yenye makazi yake pale Villa Park.
Grealish amefunga bao moja katika mechi 16 msimu huu, baada ya kufunga mara tano katika mechi 33 katika msimu wake wa kwanza akiwa City, huku mabingwa wa Serie A Milan wanatazamiwa kupeleka ombi la kushtukiza kwa Grealish kulingana na Calciomercato.
City wako tayari kumuuza mchezaji huyo, ambaye walimsajili kutoka Villa mwaka jana kwa £100 milioni, ambao ni uhamisho wa gharama kubwa zaidi wa mchezaji wa Uingereza.
Mabingwa watetezi wa Primia Ligi wako tayari kumwacha Grealish aende Milan, ili wao watumie pesa hiyo kumnunua mchezaji wa Kimataifa wa Uingereza na Borussia Dortmund, Jude Bellingham. Milan wanaweza kumnunua Grealish mwishoni mwa msimu.