Beki wa Manchester City Kyle Walker hatampa Kylian Mbappe upendeleo wowote siku ya Jumamosi wakati Taifa lake la Uingereza litamenyana na Ufaransa katika robo fainali ya Kombe la Dunia.

 

Walker Hatampa Mbappe Nafasi ya Upendeleo

Uingereza ya Southgate waliiondoa Senegal katika hatua ya 16 bora lakini wanakabiliwa na mtihani mgumu zaidi dhidi ya mabingwa hao watetezi wa 2018, ingawa Walker anafahamu vyema kuhusu tishio la nyota wa PSG, Mbappe na anasisitiza kwamba vijana wa Gareth lazima waelekeze Ufaransa kama timu na si watu binafsi.

Mchezaji huyo wa Manchester City, mwenye umri wa miaka 32, amesema: “Ni mchezaji mzuri katika kiwango kizuri kwa hivyo haitakuwa kazi rahisi, lakini kama mtaalamu unataka kucheza dhidi ya wachezaji bora na ni mmoja wa wachezaji bora zaidi Duniani ninanelewa nunachohitaji kufanya ili kumzuia.”

Walker Hatampa Mbappe Nafasi ya Upendeleo

Walker anaendelea kusema kuwa amekutana na baadhi ya wachezaji bora Duniani lakini lazima achukulie kama mchezo mwingine na lazima ampe heshima lakini sio sanam huku akisisitiza kuwa utakuwa mchezo mgumu lakini timu haiwezi kuwa mtu mmoja tu pia hatamuacha afunge kirahisi, ni Kombe la Dunia ni kufa au kupona.

Beki huyo anakabiliwa na kazi kubwa ya kumzuia Kylian Mbappe kuwa kimya siku ya Jumamosi, wakati City wamecheza na PSG katika Ligi ya Mabingwa hawakufikiria tu Mbappe na vivyo hivyo Jumamosi.

Walker Hatampa Mbappe Nafasi ya Upendeleo

“Tunamfahamu ni mchezaji mzuri na ndio maana anazingatia maswali yote. Lakini tusimsahau Olivier Giroud, ambaye amefunga mabao mengi, Ousmane Dembele na Antoine Griezmann. Kwangu mimi, maswali yote yasiwe kuhusu yeye [Mbappe]. Nashukuru ni mwanasoka mzuri lakini kuna wengine pia.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa