Fiston Mayele Mchezaji Bora Mwezi Novemba

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Kalala Mayele amechuku tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi kuu ya NBC.

 

Fiston Mayele Mchezaji Bora Mwezi Novemba

Fiston amechukua tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango bora mwezi huo na kuwa mchezaji wa kwanza mwezi huo kupiga Hat-trick kwenye mchezo ambao walikuwa wakicheza dhidi ya Singida Big Stars.

Fiston kabla ya hapo alikuwa na mabao matatu lakini baada ya kupachika mabao hayo matatu kwenye ushindi wa 4-1 wa Yanga ulimfanya awe na mabao sita na hapo baadae kupachika mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji, na Mbeya City mawili.

Jumla yakawa mabao kumi ambayo anayo mpaka sasa, na kuja kufikiwa na mshambuliaji wa Simba Mosses Phiri ambaye nae pia ana mabao kumi mpaka sasa baada ya michezo hiyo waliyocheza.

Fiston Mayele Mchezaji Bora Mwezi Novemba

Msimu uliopita Mayele alikosa kiatu cha mfungaji bora baada ya kupitwa na George Mpole bao moja, je msimu huu atachukua kiatu hicho?

Yanga ndio vinara wa ligi mpaka sasa baada ya kufikisha pointi 38 baada ya michezo 15 waliyocheza wakiwa wameshinda mechi zao 12, sare 2 na kupoteza mara 1.

 

Acha ujumbe