Beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Ibrahim Konate amesema ana furaha sana kushuhudia vita pembeni ya uwanja kati ya mshambuliaji wa timu ya Ufaransa na beki Kyle Walker katika mchezo wa robo fainali.
Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya Poland kwa jumla ya mabao matatu kwa moja huku mshambuliaji Kylian Mbappe akifunga mabao mawili. Huku timu ya taifa ya Uingereza ikifanikiwa kuitupa timu ya taifa ya Senegal kwa jumla ya mabao matatu kwa bila.Konate anaeleza anasubiri vita kati ya Mbappe kwa hamu kubwa kwasababu anasema Walker na Mbappe ni wachezaji wawili wazuri sana. Walker ni miongoni mwa mabeki bora duniani huku akiona kama Mbappe ni mchezaji mgumu sana kumzuia.
Beki Konate anaona kuna vita kubwa ambayo inaenda kutokea kwenye mchezo wa Robo fainali wa kombe la dunia siku ya jumamosi ambapo utawakutanisha wachezaji hao wenye kasi zaidi mmoja akicheza kama beki na mwingine kama mshambuliaji wa pembeni.Timu ya taifa ya Ufaransa na timu ya taifa ya Uingereza wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa robo fainali siku ya jumamosi unatarajiwa kua mchezo mkali na wenye ubora mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili.