Yanga Yaicharaza Namungo Yabaki Kileleni

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kupata alama tatu dhidi ya klabu ya Namungo Fc ya mkoani Lindi katika mchezo wa ligi ya NBC uliopigwa katika dimba la Majaaliwa mkoani Lindi.

Klabu ya Yanga iliyoonekana kutawala mchezo kwa muda mrefu ilifanikia kujipatia bao lake kwanza kupitia kwa beki wake Yannick Bangala dakika ya 40 ya mchezo baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa Natahan Nahimana na mchezo kwenda mapumziko wananchi wakiwa viongozi.yangaKlabu ya Namungo ilirudi kipindi cha pili kitofauti kidogo na kujaribu kutengeneza mashambulizi lakini ukuta wa wananchi ulikua imara zaidi na kushindwa kupata bao mpaka pale mchezo uliporudi kwa wanachi dakika ya 83 Tuisila Kisinda kuandika bao la pili la mchezo na ndio likawa la mwisho.

Wananchi wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila huku wakicheza kwa kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo na kuwafanya Namungo kushindwa kupata matokeo katika mchezo huo.yangaKlabu ya Yanga wao wanaendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi ya NBC kwa kufikisha alama 38 baada ya kucheza michezo 15 ya ligi hiyo, Klabu iyo leo imekamilisha michezo yake ya mzunguko wa kwanza na imesalia kileleni mwa msimamo na kuonesha ina nia ya kutetea ubingwa wake.

Acha ujumbe