Baada ya kuibuka na ushindi jana jumapili, kikosi cha Yanga kimeondoka leo alfajiri Dar kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namungo.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa Desemba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa.
Baada ya ushindi wa jana jumapili dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema hajafurahishwa na viwango vya wachezaji wake.

“Tulijua tunakuja kucheza na timu ambayo inaingia na mipango ya kuzuia hivyo tuliwaambia wachezaji wetu wasipoteze umakini kwani wakizuia sana watachoka.
“Tumepata ushindi ni muhimu kwetu lakini kuna baadhi ya makosa tuliyafanya kwani tunaruhusu timu pinzani itushambulie lakini tunaenda kulifanyia marekebisho.”

