Kocha wa klabu ya Napoli Luciano Spaletti haamini kama klabu yake imekua na msimu bora ambao utaisha mwaka huu kwani yeye anaiona timu hiyo ikiendelea kufanya vizuri kwa miaka mingine mbele.
Kocha Spalletti hakubaliani na mawazo ya wengi ambao wanaona kua Napoli imekua na msimu wa maajabu ambao unatokea mara moja baada ya miaka mingi kupita, Huku kocha huyo akiona hayo ni maoni tu lakini yeye binafsi anaamini wanweza kufanya vizuri zaidi miaka kadhaa ijayo.
Klabu ya Napoli watashuka dimbani kupambana na Torino wikiendi hii huku wakifanikiwa kushinda mchezo huo wanaweza kwenda kwenye mapumziko ya michezo ya kimataifa wakiwa kileleni kwa alama 21, Ikiwa alama nyingi zaidi na kuonekana kama sio rahisi kufikiwa huku ikiw aimebaki michezo 11.
Klabu ya Napoli imefanikiwa kua na msimu bora sana mpaka kufikia kuvunja rekodi mbalimbali kwani klabu hiyo haikuwahi kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini mwaka huu wamefanikiwa kufuzu hatua hiyo huku wakipewa nafasi kubwa pia ya kutwaa taji hilo.
Napoli imekua moja ya timu tishio barani ulaya kutokana na ubora wanaouonesha katika michezo yao kila siku, Kutokana na ubora huo kumemfanya kocha Spalletti kuamini inawezekana klabu hiyo kuendelea kufanya mambo makubwa kwa miaka mingine zaidi baada ya msimu huu kumalizika.

