Beki wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika klabu ya Ac Milan ya nchini Italia Fikayo Tomori amesema anahakikisha anapambana kwa kiwango kiukbwa ili aweze kuitwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki Euro 2024.

Beki huyo amekua katika ubora wa hali ya juu katika klabu ya Ac Milan na kuisaidia klabu hiyo kuweza kbeba taji la Serie A baada ya miaka 11, Huku akiwa nguzo na mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Milan chini ya Stefano Pioli.tomoriFikayo Tomori alikosekana kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kilichoshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka huu, Kitu ambacho beki huyo hataki kijirudie kwa mara nyingine.

Beki huyo anasema kila siku yeye anahakikisha aanaimarika japo kuna vitu vya tofauti vinatokea, Lakini yeye anasema apambana zaidi ili kuweza kuwepo kwenye michuano ya Euro mwaka 2024 baada ya kukosekana Qatar kwenye michuano ya kombe la dunia.tomoriBeki Fikayo Tomori kwasasa akiwa na miaka 24 bado anaendelea kuonesha ubora mkubwa kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Serie A klabu ya Ac Milan, Hivo watu wengi kuamini ataitwa kwenye kikosi cha Uingereza kama ataendelea kuonesha ubora huo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa