Keylor Navas Kuendelea Kupambana Real

Golikipa wa Real Madrid, Keylor Navas amesaini mkataba mpya utakaomfanya kuendelea kuwepo klabuni hapo hadi Juni  2021. Nyota alikuwa anahusishwa na klabu ya Arsenal, lakini Unai Emery alikanusha taarifa za kuhitaji kumsajili, sasa ameongeza mkataba wake kusalia Real Madrid.

Hatma ya golikipa huyu pale Real Madrid ilikuwa ikitia wasiwasi kufuatia kupungua kwa mda wa kucheza soka klabuni hapo toka alipofika Thibaut Courtois na Sanriago Solari kuteuliwa kuwa kocha mkuu. Dakika zake mchezoni zimezidi kupungua zaidi siku hadi siku.

Amesaini kuendelea kuwepo
Keylor Navas Kuendelea Kupambana Real
Keylor Navas

Wiki kadhaa zilizopita golikipa huyu aliamua kumwaga wino kuongeza mkataba wake, sasa mkataba huu utamlipa paundi milioni 5 kwa kila msimu hadi mwaka 2021.

Dirisha la uhamisho la mwezi Januari linamuacha nyota huyu klabuni hapo akitarajia kupambana na hali yake ili angalau aweze kujiongezea mda zaidi wa kucheza.

Jarida la Marca linaripoti kuwa yeye [Navas] na familia yake wameshauzoea na kufuhahia maisha ya mji wa Madrid. Inaweza kuwa ni moja ya sababu katika msukumo wake wa kuongeza mda zaidi wa kuwepo klabuni hapo.

2 Komentara

    Pambana mzee.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.