Manchester City imerejea kwa kishindo kwenye njia ya ushindi baada ya kuicharaza vikali Manchester United kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa derby ya Manchester. Erling Haaland na Phil Foden waliibuka mashujaa wakifunga mabao yaliyowapa City ushindi dhidi ya mahasimu wao wa jiji.
Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo kabla ya mapumziko ya kimataifa, Manchester City walionekana wenye njaa ya ushindi tangu dakika za mwanzo. Phil Foden aliongoza mashambulizi kwa ustadi mkubwa na kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 18 akimalizia kwa ustadi krosi ya kuvutia kutoka kwa Jeremy Doku aliyewatesa mabeki wa United upande wa kulia.
Manchester United walijaribu mara kadhaa kufika langoni kwa kipa mpya wa City, Gianluigi Donnarumma, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Italia alisimama imara. Alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Bryan Mbeumo katika kipindi cha pili na kuonyesha kuwa yuko tayari kwa changamoto za Ligi Kuu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa



