Mbappe Achana Rekodi Nyingine

Mbappe ameweza kufikia rekodi nyingine iliyowahi kuwekwa na raia wa Brazil, Ronaldo Luís Nazário de Lima ya ufungaji wa magoli katika michuano mikubwa kabisa barani Ulaya ya klabu bingwa. Akiwa na PSG amekuwa moto usiozimika kutokana na uwezo wake mkubwa alionao ndani ya uwanja kwa kutumia uwezo wake kuadhibu timu nyingi anazokutana nazo uwanjani katika hatua zote.

Mshindi huyo wa kombe la dunia na tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika fainali za kombe lile, ameweza kuifikia rekodi iliyowahi kuwekwa na De Lima miaka ya nyuma. Mbappe mwenye miaka 20 tu ameweza kuifikia rekodi hiyo kwa kucheza mechi chache tu ambazo tayari zimemfanya aweze kuwa bora kwa namna ya pekee ndani ya kipindi kifupi na michezo michache aliyoicheza kwa sasa.

Ikoje?

Nyota huyo wa Paris Saint-Germain ameweza kufikia rekodi ya kufunga mara 14 katika mechi zake 24 alizocheza hivi karibuni, wakati Ronaldo aliweza kufikia rekodi ya magoli 14 katika mechi 40 alizozicheza. Tayari kwa hatua hiyo ambayo ameifikia ni kubwa sana na haipingiki anafanya makubwa sana kwa wakati uliopo.

Mbappe ana wakati mrefu sana kuendekea kucheza soka na safari yake bado ipo na ubichi wake kabisa. Kwa sasa anafukuzia rekodi za akina Cristiano Ronaldo (121) na Lionel Messi (106) ambao wamefunga magoli hayo katika michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya. Na tayari mwanga unaonekana kumulika maisha yake ya kisoka kwa sasa kuelekea kuvunja rekodi hizo.

Mbappe kwa sasa ni mchezaji halali wa PSG baada ya kusaini kandarasi yake msimu uliopita, baada ya kuwa kwa mkopo ndani ya klabu hiyo kutoka Monaco. Kwa wakati uliopo mchezaji huyo ndiye anayeonekana kuja upya katika ushindani wa kisoka baada ya utawala wa Ronaldo na Messi.

Mshindi huyo wa kombe la dunia alikuwa moto ndani ya kikosi kilichoumana na United baada ya kuwafunga miamba hao wakiwa nyumbani kwao. Pamoja na kikosi chao kuwakosa Neymar na Edinson Cavani ambao walipata majeraha katika kipindi cha ukingoni kabisa cha kuelekea mechi hiyo lakini kukosekana kwao hakukuonekana kabisa ndani ya kikosi hicho kilichokuwa imara sana.

Katika mechi hiyo ambayo Mbappe alijipatia umaarufu zaidi; Di Maria naye alikuwa katika ubora wake kwa kutoa pasi za magoli yote mawili lakini kitu ambacho hawezi kukisahau ni kuzomewa na mashabiki wa klabu hiyo ambao waliwahi kuwa naye klabuni hapo. Pia, Sanchez hawezi kuusahau usiku ule baada ya kupotea kabisa uwanjani na kutoonesha kile kocha alichomtuma kukifanya. Kwa mwenendo wa Mbappe kwa kipindi kijacho atashuhudiwa akinyanyua tuzo nyingi sana zikiwemo zile za Ballon d’Or.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.