Huyu ndiye Lionel Messi, fundi wa Barcelona ambaye asipokuwepo tu dimbani pengo lake halizibiki! Bwana huyu ametandika Hat-Trick yake ya 50 kwenye gemu dhidi ya Sevilla jana wakipata ushindi wa bao 2-4.
Wenyewe wanasema ng’ombe hazeekimaini! Basi tunaweza kusema hivi kwa fundi huyu ambaye kila uchao yeye anaendelea kuwa wa moto licha ya umri wake kuendelea kumtupa mkono.
Tofauti na mastaa wengi ambao katika umri wake wa miaka 31 wamekuwa wakipoa taratibu wakati wengine wakiwa wameshaachia gozi kwa vijana wanaochipukia, Messi yeye anaenda sawa na kuwatupa vijana.

Wakati anafikisha Hat-Trick ya 50, nyota huyu tayari ametia nyavuni jumla ya magoli 650. Magoli 585 ni zawadi aliyowapa Barca kwa kipindi alichokuwepo klabuni hapo na magoli 65 ni aliyowachapia timu ya taifa ya Argentina.
Mpaka sasa yeye ni kinara wa La Liga kwenye magoli akiwa ametupia 25 kwa msimu huu, amemtupa Suarez aliyepo nafasi ya pili kwa magoli 9 zaidi huku Cristhian Stuani akiwa ametandika magoli 13 kwa klabu ya Girona akiwa nafasi ya 3.
Fundi messi kwa michuano yote msimu huu amecheka na nyavu mara 33 katika gemu 32, magoli 6 ni ya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nani wa kumkamata Messi LaLiga!



Povel tz
Messi noma sana