Msimu Mpya: Ratiba ya La Liga

Siku kadhaa nyuma ratiba ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya huko Hispania, La Liga 2017/18 ilitoka na gemu za kwanza zitasakatwa wikiendi ya kuanzia Agosti 18. Katika wikiendi hiyo wale Mabingwa ambao ni klabu ya soka ya Real Madrid wataanza utetezi wao wakiwa ugenini kukipiga na Deportivo La Coruna!

Nayo timu ya pili, Barcelona itaanza ikiwa kwao Nou Camp kwa kumenyana na Real Betis. Katika ratiba hiyo ni kuwa vigogo hao wawili watamenyana uso kwa uso kwenye El Clasico wikiendi ya kuanzia Desemba 20 dimbani Santiago Bernabeu na kurudiana kule Nou Camp wikiendi ya kuanzia Mei 6 kwenye hatua ya Raundi ya 36 ambapo zitakuwa zimebaki mechi 2 tu ili ligi iishe.

Wanaokamatia nafasi ya 3, klabu ya soka ya Atletico Madrid wataanza hekaheka zao wakiwa nyumbani kwao dhidi ya Girona FC wakati Sevilla wakicheza na Espanyol, ni hakika kuwa hupaswi kupitwa na hii!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.