Sharapova Amchapa Bingwa Mtetezi!

Bingwa mtetezi wa michuano ya Australian Open Caroline Wozniacki ameshindwa kuchomoka kwa bingwa mara tano wa Grand Slam Maria Sharapova na kukubali kutolewa nje ya michuano hiyo.

Mrusi huyu, Sharapova amemkalisha Wozniacki kwa ushindiwa seti 6-4 4-6 6-3 akitoboa kuingia raundi ya 4. Wozniacki mbaye ana umri wa miaka 28 alianza vyema kwa kuongoza kwa seti ya kwanza 4-1 kabla Sharapova hajarejea kwa kishindo.

Mwanadada huyu anasema mchuano huu kwake haukuwa mgumu, zaidi aliuona kama kiburudisho kwake!
“Sijacheza mechi nyingi mwaka uliopita, hasa mechi dhidi ya wachezaji wakubwa na hawa ndio ninaojifua kwa ajili yao, hivyo inalipa saba kupata ushindi.” -Sharapova

Sharapova Amchapa Bingwa Mtetezi!
Sharapova {Kushoto}, Wozniaki {Kulia}

Sharapova anajitahidi kurejea kwa kasi baada ya kupata vikwazo kadhaa siku za nyuma, ikiwa ni pamoja na kufungiwa kwa sababu ya matumizi ya madawa kinyume na taratibu zinazotawala mchezo huo.  Wozniacki alikuwa ni mmoja ya wachezaji ambao walikuwa wanapinga suala alilolifanya mwanadada huyu, lakini baada ya gemu wamepeana mkono wa pongezi!

2 Komentara

    Madawa ya kulevya sio mazur

    Jibu

    Habar njema sana 👍

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.