Xavi na Barca Yake Kizungumkuti

Klabu ya Barcelona mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga hawaeleweki chini ya kocha wao Xavi Hernandez. Hii imekuja kutokana na matokeo ya kusuasua wanayopata klabu hiyo.

Barcelona jana wamelazimishwa sare na klabu ya Valencia katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania, Huo ukiwa mchezo wa tatu mfululizo bila kupata matokeo ya ushindi katika michuano yote.xaviMabingwa hao watetezi chini ya kocha Xavi jana wamecheza mchezo wa tatu bila kupata matokeo ya ushindi ambapo katikati ya wiki wamepoteza  dhidi ya Royal Antwerp kwenye ligi ya mabingw aulaya, Huku wakitoka kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Girona wikiendi iliyopita na jana wametoka sare na Valencia.

Hali inaonekana sio hali ndani ya klabu hiyo kutokana na matokeo timu hiyo inayopata, Huku hali hii ikianza kuzua hofu kwa mashabiki wa klabu hiyo kua huenda klabu hiyo ikashindwa kutetea ubingwa wake ambao waliubeba msimu ulimalizika.xaviMpaka sasa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wameonekana kutoridhishwa na muenendo wa timu yao, Huku wakioneka kama kocha Xavi hatoshi ndani ya timu hiyo anapaswa kupisha kocha mwenye uwezo zaidi aweze kuwarudisha kwenye zama zao za ubora.

Acha ujumbe