Klabu ya Tottenham imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono unaowafanya waendelee kujizatiti kileleni mwa ligi hiyo hadi sasa kwa kuweza kuwapiga Fulham 2-1; ushindi unaowafanya wakae vizuri katika nafasi yao ya tatu kwenye ligi jiyo inayoonekana kuzidi kupendeza kadri siku zinavyozidi kwenda na inavyozidi kuelekea ukingoni mwake tangu ianze kutimua vumbi.
Asante kubwa kwa Harry Winks aliyeokoa jahazi hilo lililokuwa linaelekea kuzama kwa kufunga goli katika dakika za lala salama; kitu ambacho kingepelekea mechi hiyo kuisha kwa sare. Ameipa timu hiyo matokeo sahihi kabisa ambayo kila shabiki wa timu hiyo ameridhika kwa kiasi kikubwa kuyapata.
Kiungo wa Uingereza aliyeisawazishia timu yake baada ya kutangulizwa Delle Alli [22] aliweza kupata jeraha katika kifundo chake mnamo dakika ya 86 ya mchezo kitu kilichomfanya kutolewa uwanjani na kwenda kufanyiwa matibabu ya awali.
Kikosi hicho kwa sasa kinaweza kuwa na wakati mgumu ikizingatiwa kwamba idadi yake kubwa ya wachezaji tegemezi hawapo; na kama ripoti za kitabibu zitatoka endapo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu basi itakuwa ni hatari zaidi kwa mwalimu wa kikosi hiki kuweza kutetea nafadi yake hiyo ya juu.
Harry Kane yupo majeruhi, naye ikumbukwe aliumia katika dakika za lala salama katika mechi yao na Manchester United. Na kuongeza idadi ya majeruhi ndani ya kikosi hicho, tena hiyu naye ameongezea idadi ya majeruhi ndani ya timu hiyo. Inawwza kuwa ni dalili mbovu kwa Spurs japo bado wana kikosi kipana pia.
Mbali na hao pia kuna wachezaji wengine kama kiungo wa timu hiyo: Sissoko ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili; ambaye naye aliumia katika mechi iliyopigwa dhidi yao na Manchester United.
Mchezaji wao mwingine tegemezi Son Heung-Ming ambaye yupo katika majukumu ya kimataifa kuisaidia timu yake katika mivhuano ya kombe la nchi zinazopatikana upande wa bara la Asia, hivyo hatakuwepo ndani ya kikosi hicho kwa takribani wiki tatu. Hadi sasa wachezaji tegemezi zaidi ya watano Lucas Moura akiongezwa kwenye kundi hilo; hawapo katika kikosi hicho cha kwanza.
Spurs wapo nafasi ya tatu wakiwa alama tisa nyuma ya Liverpool anayeongoza ligi hiyo kwa sasa. Japo majeraha hayo yanaonekana kutomtisha mwalimu wa kikosi hicho akiamini kwamba hayawezi kuwa makubwa sana; japo kwa sasa anasubiri ripoti kutoka kwa madaktari wa timu hiyo juu ya maendeleo ya mchezaji huyo.


Povel
Gud news