UEFA: Nani Kuondoka Leo?

Macho na masikio yote kwenye mtanange wa leo ni nani ataendelea kusalia kwenye michuano hiyo na nani atafungashiwa safari yake ya ushiriki ndani ya michuano hiyo. Miamba wa soka watakuwa viwanjani leo kusaka tiketi ya ushiriki wa nusu fainali ya michuano hiyo huku kukiwa na kila dalili kwa mechi moja kuonekana kabisa nani atafuzu mechi hiyo.

Liverpool watakuwa uwanjani kuumana na FC Porto katika mechi ambayo inaonekana kuwa nyepesi lakini inawataka Liverpool kuwa makini sana maana kwenye soka lolote hutokea na soka siku zote ni mchezo wa makosa na kosa linapofanywa hupelekea mpinzani kupata nafasi ya kuchukua ushindi.

Katika mechi ya awali, Liverpool walishinda mechi yao kwa magoli 2-0 japo ushindi huo kwa hakika katika michuano hii sio kitu chochote kwani lolote huweza kutokea maana mapinduzi ya soka yana nafasi kubwa sana kutokea pale timu inapoamua kupambana kurejesha heshima yake hususan wakiwa nyumbani.

Klopp ataendelea kumkosa Chamberlain kwenye kikosi chake japo sio chaguo lake kubwa ndani ya kikosi kazi chake. Jambo ambalo linaonekana kuwa ahueni kwake kuendelea kufanya vizuri zaidi mbele ya Porto ambao kwa hakika hawapigiwi upatu sana kuchukua ushindi mbele ya Klopp na vijana wake.

Katika mechi inayotupiwa jicho kubwa ni ile ya Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao kwa hakika ni watani wa ligi moja na kila mmoja anamjua mwenzake kwa kipindi kirefu. Lazima mmoja kati yao aondoke na kumuachia mwenzake nafasi ya kusonga mbele baada ya kuwa katika kipindi kizuri na nafasi nzuri kwenye ligi.

City anapigana kushinda makombe yake yote ambayo anashiriki msimu huu lakini bado ana vigingi vikubwa kuruka hadi kufikia hatua hiyo. Ametumia kiasi kikubwa cha fedha kusajili hivyo analazimika kuonesha thamani ya hiyo fedha kwa kunyanyua mataji mengi zaidi anayoshiriki kuliko kawaida.

Spurs bado wapo katika nafasi nzuri kusonga mbele kutokana na kutokuruhusu kufungwa goli lolote wakiwa nyumbani na wao kuwa mbele kwa goli moja linalowapa kipaumbele zaidi kwenda kutafuta goli la ugenini ili waweze kujiweka pazuri zaidi mbele ya Manchester City wenye njaa ya vikombe.

Spurs wanaenda uwanjani wakiwa hawana huduma ya nyota wao na mshambuliaji anayeogopwa, Harry Kane ambaye aliumia kwenye mchezo wao wa awali pale klabu hizo mbili zilipokutana. Japo wachezaji waliopo wanatosha kabisa kuwapa somo City na wakaelewa nini maana ya ushindani na kipi wakifanye kuulinda ushindi huo. Nafasi bado ipo kwa wote wawili kusonga mbele kwa sababu mmoja yupo nyumbani na mwingine yupo ugenini lakini mbele kwa goli moja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.