Mabingwa wa Italia wameshindwa kutoboa kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya -UCL baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Ajax.
Juventus wamejikuta wapo nje ya michuano hii baada kulazimisha sare ya bao 1-1 kwenye mzunguko wa kwanza wa michuano hii pale dimbani Allianz ikiwa ni gemu ya nyumbani, kichapo cha gemu ya pili kimewaacha wakipungia mkono ubingwa wa mwaka huu.
Hata hivyo, klabu hii bado ina matumaini makubwa zaidi katika ligi ya Mabingwa Ulaya kwa siku za usoni, wanatarajia watakuwa wameunasa ubingwa ndani ya miaka 2 tu baada ya kukwama msimu huu.
Juventus walikuwa na matumaini makubwa mno ya kuutwaa ubingwa wakiwa na nyota wao cristiano Ronaldo waliyemnunua kwa pesa nyingi paundi milioni 112, lakini matumaini yao yameenda tofauti kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo kwenye michuano hii.
Bernardeschi anaamini hamu yao ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya -UCL itatulizwa katika kipindi cha hivi kiaribuni.

