Raisi wa UEFA Aleksander Caferin amesema mashindano ya UEFA yanaweza kumaliziwa watu wakiwa ndani kuliko kukatisha kabisa mashindano hayo, Lakini kama Korona (Covid19) itaendelea mpaka mwezi September basi itabidi tu mashindano hayo yakatishwe.
“Tuna subiri kuona kitakacho endelea duniani hususan kwenye bara la ualaya, Mpira si chochote bila mashabiki na ni afadhali kucheza kukiwa na mashabiki kuko wasiwepo kabisa, tatizo ni kwamba mpira hauwezekani bila mashabiki.”
“kwahiyo sasa ni lazima tucheze mpira lakini mashabiki wabaki nyumbani na wata angalia mpira wakiwa nyumbani kwa njia ya televisheni kwa maana ya kwamba ilaleta taswira chanya kwenye familia kwakua mpira ni mchezo wa furaha.

UEFA inazingatia mapendekezo ambayo yataona fainali ya Ligi ya Mabingwa ikichezwa Agosti 29, miezi mitatu baadaye kuliko ilivyopangwa awali. Awali Fainali ya Ligi ya Mabingwa ilikuwa imepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk huko Istanbul Mei 30.
Moja ya mapendekezo mapya ambayo UEFA itajadili wiki ijayo, fainali itasogezwa mbele hadi Jumamosi, Agosti 29 kwenye uwanja huo wa nchini Uturuki. Kwa upande wa Fainali ya Ligi ya Europa ambayo ilipangwa kuchezwa Gdansk Mei 27 sasa inaweza kuchezwa Jumatano, Agosti 26.
Ndugu msomaji kila siku ya juma tatu, juma tano na ijumaa saa 7:00 kamili tutakuletea makala maalum kuhusu UEFA.


Elika
Ni habari njema pia.