katika ulimwengu wa soka kuna maajabu mengi sana, Zipo familia zenye bahati zaidi kiasi cha ndugu wa familia hizo kushiriki katika michezo na kua maarufu sana kupitia michezo hiyo, Hapa tuna familia chache tu za wanasoka maarufu ambao kama familia wameshiriki katika mchezo wa soka kimataifa na dunia ikawatambua kwa uwezo wao.
Eden na Thorgan Hazard

Wanandugu hawa wa familia ya Hazard wana ndugu yao anaitwa Kylian ambae alicheza kwa ubora mkubwa sana katika kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia kwa taifa la ubeligiji. Hazard kwasasa anakipiga katika timu ya Real Madrid akiishi na mdogo wake Kylian huku Thorgan akikipiga timu inayo shiriki ligi kuu ujerumani ya Borussia Monchenglaqdbach.
Gary na Phil Neville

Iwe umewapenda ama kuwachukia ndugu hawa wanatajwa kua ndio familia maarufu zaidi katika historia ya soka la kimataifa, wawili hao wote walikua ni wachezaji wa Manchester United kwa miaka ya 90 , Gary anaweza kua maestaafu kwa ukimya kidogo lakini Phill alikua bora zaidi kumliko kaka yake,
Rafael na Fábio da Silva

Watoto hawa wa Kibrazili sio tu ndugu wa baba mmoja kama walivyo phill na gary, wao ni mapacha, na wamekua ni moja ya ndugu wanao vutia zaidi kwenye historia ya soka. Wote wawili wamekulia Manchester United kabla ya kusambaratika, Rafael alifikia mwisho wa utumishi wake pale United baada ya majeraha 27 yaliyoharibu kabisa malengo yake ya kuendelea kubaki United iliyokua chini ya mzee Ferguson kwa wakati ule.
Jérôme na Kevin-Prince Boateng

Tukizungumzia vituko vya familia za soka basi hatuwezi kuacha kuzungumzia familia ya Kelvin Prince na Jerome Boateng ambapo wanafamilia hawa walicheza timu mbili tofauti za taifa. Kuna mambo mengi ya kushangaza kwenye familia hiyo, kaka mkubwa wa familia hiyo anatajwa kua ndio mwenye kipaji zaidi, huku ndugu yao wa kati (kelvin prince) amekua maarufu zaidi wakati jerome ndie mwenye taji la kombe la dunia na ubingwa wa ulaya.


Furahav
Hii habari iko vizuri
Issa
Familia ya hazard nihatari