UEFA wamethibitisha kuwa kesi ya Ronaldo imepatiwa meza ya kusikiliza maswala ya kinidhamu juu adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Ronaldo kwenye gemu dhidi ya Valencia jana.
Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29 baada ya muamuzi Felix Brych na msaidizi wake kuamua kuwa alistahili kadi hiyo kwa kumvuta nywele mlinzi wa Valencia.
Kesi inayotarajiwa kusikilizwa ni inalenga kadi ya moja kwa moja aliyopewa Ronaldo kama adhabu na uhusiano wake na kosa analodaiwa kulifanya huku wakitazama uhalisia na adhabu anayostahili.
Kesi hii inatarajiwa kusikilizwa alhamisi ijayo ya Septemba 27, kusikilizwa kwa kesi hii ni utaratibu ambao hautamuongezea adhabu Ronaldo, ila ukweli zaidi utapatikana baada ya kamati ya nidhamu kusikiliza kesi hiyo.
Baadhi ya ripoti zilidai kuwa Juventus wanatarajia kukata rufaa kuhusu adhabu hiyo aliyopewa nyota wao wakidai ni kulikuwa na kasoro.


Povel tz
Gud news