Wakati ikiwa ni suala la muda tu kabla ya kumuona Darwin Nunez kwenye jezi ya Liverpool, inasemekana Manchester United waligomea mchongo.

Inasemekana, mpaka ijumaa ya wiki iliyopita, United walikua mazungumzoni na wakala wa Nunez. Kikwazo kikubwa kilikua ni gharama aliyowekewa mchezaji huyo. Benfica walitaka €100M huku The Red Devils wakimuona ni mchezaji mwenye thamani ya €70M.

Utofauti wa thamani ya mchezaji uliwafanya United waamue kuachana na usajili wa Nunez na kujiweka kando wakiwaacha Liverpool kwenye mchakato ambao, unaelekea tamati muda sio mrefu.

United

Pengine hii ni ishara nzuri kwa The Red Devils ambao, wamezoeleka kama timu inayomwaga pesa sokoni bila kujali thamani halisi ya mchezaji. Wakitaka jambo lao, linakuwa. Utawala wa Richard Arnold unaonesha picha ya tofauti msimu huu.

Erik Ten Hag alimtaja Nunez kama miongoni mwa wachezaji ambao angewahitaji kwenye kikosi chake lakini, inaripotiwa kuwa, kwa dau lililokuwa limewekwa na Benfica, haoni kama amepoteza kitu kwa M16 kuacha kumsajili. Badala yake, anaamini ni uelekeo sahihi wa klabu kutumia pesa katika sehemu sahihi na yenye uhalisia ndani yake.

Je, Manchester United watakuja kujilaumu kwa kumkosa Nunez au Liverpool wataambulia kipigo kwa kumsajili mchezaji aliyeng’ara kwa msimu mmoja pekee?


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa