Tetesi zinasema, Juventus wana uhakika mkubwa ya kumsajili Paul Pogba, 29 bure kutoka Manchester United. Kiungo huyo mfaransa amekubali kusaini mkataba wa miaka minne.

Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 30, ameamua kutafuta changamoto mpya na anajiandaa kutimka Brentford. Vilabu vya Tottenham Hotspur na Manchester United vinammendea nyota huyo.

Tetesi zinasema, Manchester United wanamfukuzia winga wa Brazil Antony, 22, kutoka Ajax, na kiungo wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kutoka Barcelona.

 

Frenkie De Jong Xavi

Tetesi zinasema, Chelsea wanakaribia kumnasa kipa Mmarekani Gabriel Slonina, 18, kutoka Chicago Fire baada ofa ya Real Madrid ya £8.5m kukataliwa.

Tetesi zinasema, Leeds United wanaongoza katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa New York City mwenye miaka 23 muargentina Valentin Castellanos.

Kama mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, ataondoka Sevilla na kujiunga na Chelsea, basi Barcelona itaelekeza nguvu zake kumsajili Kalidou Koulibaly, huku Napoli wakitaka angalau £34.1m kwa ajili ya mlinzi huyo Msenegal.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Ofa ya Paris St-Germain ya £34.1m kwa ajili ya mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar imekataliwa, lakini Inter Milan wanaweza kukubali kuchukua £51.2m kwa ajili ya mlinzi huyo mwenye miaka 27.

Klabu ya Argentina ya River Plate imewasiliana na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 35 ili ajiunge bure anapomaliza mkataba wake na na klabu ya Atletico Madrid msimu huu.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa