Andy Murray amekosa taji lake la kwanza la uwanja wa nyasi tangu ashinde Wimbledon mnamo 2016 baada ya kufungwa na Matteo Berrettini katika Fainali ya Stuttgart Open leo [Jumapili].

Mchezaji huyo namba moja wa zamani alikumbana na kichapo cha 4-6 7-5 3-6 kutoka kwa Muitaliano huyo katika kile kilichokuwa ni kipigo chake cha pili katika fainali 10 za uwanja wa nyasi.

 

berrettini, Matteo Berrettini Bingwa Stuttgart Open., Meridianbet

Pengine wasiwasi mkubwa zaidi ulikuwa kwa Murray kuhitaji matibabu kutoka kwa physio mara mbili katika seti ya tatu.

Berrettini alikuwa akicheza katika mchuano wake wa kwanza tangu Machi kutokana na jeraha la mkono wa kulia ambalo lilimweka nje wakati wa msimu wa udongo.

“Imekuwa wiki ya kuvutia. Niliifurahia sana. Ningependa kumpongeza Matteo na timu yake kwa wiki nzuri,” Murray alisema katika mahojiano.

 

“Amerejea kutoka kwenye upasuaji na si rahisi. Alicheza vizuri sana leo na alistahili ushindi. Hatimaye, asante kwa timu yangu hapa na timu yangu nyumbani.” aliongeza Murray.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa