Klabu ya Everton imethibitisha kumteawa Frank Lampard kuwa kocha mpya wa klabu hiyo huku akipewa mkataba wa miaka miwili na nusu kuingoza klabu hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea alifanyiwa interview siku ya Ijumaa jijini London, akiwa na watahiniwa wengine ambao walikuwa wanawania nafasi ambao ni Vitor Pereira na msimamzi wa timu aliyepita Duncan Ferguson.

Miliki na mwenyekiti wa klabu ya Everton Bill Kenwright na wajummbe wa bodi walilipitisha jina la Frank Lampard kuwa mrithi wa Rafael Benitez siku ya leo Jumatatu na kulitangaza.
Frank Lampard alisema haya wakati alipotangazwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo, “ni heshima kubwa kwangu kuiwakilisha klabu kubwa na kuwa sehemu ya utamuduni wa klabu ya Everton, nina shauku kubwa ya kuanza sasa.
“Baada ya kuzungumza na mmiliki, mwenyekiti na wajumbe wa bodi, niliziona hisia zao nashauku, na natumai nao waliweza kuona shauku yangu ni kwa jinsi gani niilikuwa nahitaji kufanya kazi pamoja nao.
“Ujume wangu wa kwanza kwa wachezaji utakuwa ni kufanya hili kwa pamoja, tutajitahidi kufanya kazi na najua mashabiki watakuwa nyuma yetu kutusiadia.”
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


