Fulham Kumchukua Jimenez

Klabu ya Fulham imefikia pazuri kwenye mazungumzo ya kumchukua mshambuliaji wa klabu ya Wolverhampton Wanderers Raul Jimenez raia wa kimataifa wa Mexico.

Fulham chini ya kocha Marco Silva inataka kuhakikisha msimu ujao wanakua kwenye ubora mkubwa na kupanda zaidi ya nafasi waliyokua msimu uliomalzika na ndio sababu wanaongeza mtu katika safu yao ya ushambuliaji.fulhamTaarifa zinasema Wolves wamekubali kiasi cha paundi milioni 5.5 kutoka kwa klabu ya Fulham kwajili ya kumuachia mshambuliaji wake Raul Jimenez ambaye atajiunga na klabu hiyo hivo karibuni.

Raul Jimenez alikua anatakiwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia lakini vyote amevipiga chini na ameamua kubaki ndani ya ligi kuu ya Uingereza ambapo msimu ujao atakua chini ya kocha Marco Silva na sio Julien Lopetegui.fulhamFulham baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Wolves kwa Jimenez lakini klabu hiyo pia imefanikiwa kumbakiza winga wake raia wa kimataifa wa Brazil Willian ambaye mkataba wake uliisha na sasa wamefanikiwa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.

Acha ujumbe