Klabu ya Arsenal inamatumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus lakini timu hiyo imewapa ofa Chelsea kumsajili mchezaji huyo.

Jesus amekuwa katika orodha ya kwanza ya washambuliaji wanaowindwa na meneja Mikel Arteta pale Arsenal tangu majira ya baridi lakini imekuwa ngumu kufanya hivyo.

 

jesus, Gabriel Jesus Awaweka Vitani Arsenal, Chelsea., Meridianbet

Arteta ambaye amewahi kufanya kazi pamoja na Jesus wakiwa Etihad alitarajia kujiunga na miamba hiyo ya Emirate licha ya klabu hiyo kushindwa kijihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.

Manchester City wanatarajia dau la angalau £50m kwaajili ya mshambuliaji huyo lakini Arsenal wanaweza kutoa kiasi cha £40m tu kwaajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Kulingana na jarida la Telegraph, City wametoa ofa kwa klabu ya Chelsea kumsajili mchezaji huyo ili kuweza kupata kiasi cha pesa wanachokihitaji zaidi ya kile ambacho Gunners wamekitoa.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa