Mchezaji Mpya wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Uholanzi Coady Gapko amefurahishwa na mchezo wake wa kwanza akiwa ndani ya jezi za Liverpool.
Coady Gapko alicheza mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu ya Liverpool jana katika mchezo wa kombe la FA. Klabu ya Liverpool iliwakarabisha mbwa mwitu klabu ya Wolves katika dimba lake la nyumbani na mchezo kuisha kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.Mchezaji huyo alionesha kiwango kizuri katika mchezo huo ambapo klabu ya Liverpool ililazimishwa sare na klabu ya Wolves ikiwa nyumbani katika dimba la Anfield. Mchezaji huyo anasema amefurahia kucheza mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliimbia tovuti ya klabu hiyo kua alifurahia namna ambavyo alicheza katika mchezo huo, Lakini anaamini kuna madhaifu pia aliyaonesha ambayo anasema ana uwezo wa kuyafanyia kazi ili kufanya vizuri zaidi siku za mbeleni.Coady Gapko pia ameeleza kua katika mchezo wa jana wao kama timu walicheza vizuri lakini hawakupata bahati ya kupata matokeo ya ushindi kwakua hawakufunga magoli ya kutosha. Gapko anawaasa wachezaji wenzake wanahitaji kua umakini mkubwa kuelekea mchezo wa marudiano katika dimba la Molineux.