Mshambuliaji wa klabu ya timu ya taifa ya Uholanzi anayekipiga klabu ya PSV Eindhoven ya nchini humo Coady Gapko ameweka wazi ataifikiria klabu ya Manchester United kama itamfata.
Nyota huyo ambaye amekua namsimu mzuri sana kuanzia kwenye klabu yake mpaka sasa kwenye timu ya taifa ya Uholanzi ambapo amekua nguzo muhimu kwenye kikosi cha kocha Louis Van Gaal kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.Coady Gapko sasa amefunga mabao matatu kwenye michuano ya kombe la dunia na kuzifanya timu mbalimbali kuanza kumfatilia kwa karibu kutoka na ubora ambao anaendelea kuonesha mchezaji huyo kwenye michuano hiyo.
Mchezaji huyo alipoulizwa kuhusu kujiunga na Man United ambayo inahusishwa nae ka karibu “Sijaskia kuhusu Man United bado. Kama watakuja, Nitafikiria na mungu akisaidia. Nilifikiri kuhusu Man United Msimu ulimalizika, Lakini kama haikutokea sijui tena kuhusu jambo hilo”Coady Gapko ni mchezaji aliekua anafatiliwa kwa karibu na klabu ya Manchester United kwenye dirisha la usajili lililopita lakini dili iliharibika mwishoni kabisa. Lakini mashetani hao wekundu wanaonekana kurudi kwa kasi na kuhitaji saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi.