Kinda wa kimataifa wa Uingereza ambaye alikua anakipiga ndani ya klabu ya Everton Anthony Gordon amekamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya soka ya Newcastle United.
Klabu ya Newcastle United imefanikiwa kukamilisha dili la mshambuliaji Anthony Gordon kutoka Everton kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 40 ili kuweza kupata saini ya nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye wamekua wakimuwinda.
Mshambuliaji huyo ambaye alikua anawindwa na vilabu kadhaa nchini Uingereza tangu dirisha kubwa lililopita kwenye majira ya joto ikiwemo klabu ya Chelsea, Lakini klabu ya Newcastle ambao wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ndio waliofanikiwa kunasa saini ya nyota huyo.
Taarifa za ndani kutoka klabu ya Everton zinaeleza kua klabu hiyo haikua imepanga kumuachia Anthony Gordon kwenye dirisha hili kama ambavyo hawakutaka kumuachia kwenye dirisha lililopita, Lakini mshambuliaji huyo ndio amelazimisha kuondoka klabuni hapo.
Anthony Gordon anaelezwa kusaini dili la muda mrefu kuitumikia klabu ya Newcastle United kuanzia msimu huu wa 2022/23, Mchezaji huyo atakua amekamilisha vipimo vya afya ndani ya masaa 24 au 48 yajayo na kua mchezaji rasmi wa klabu ya Newcastle United.

