Kiungo wa kimataifa wa Morocco Azzedine Ounahi anayekipiga katika klabu ya Angers inaelezwa anakaribia kujiunga na klabu ya Olympique de Marseille ya nchini Ufaransa.
Azzedine Ounahi amekua kwenye rada za vilabu mbalimbali barani ulaya kutokana na ubora mkubwa ambao ameuonesha katika michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana 2022, Na klabu ya Mareseille inaonekana kukaribia kunasa saini ya mchezaji huyo.
Klabu ya Olympigue de Marseille imeonekana kushinda vita dhidi ya vilabu kadhaa kunasa saini ya nyota huyo ambaye anafanya vizuri kunako ligi kuu ya Ufaransa, Kiungo Ounahi sasa atakwenda kuitumikia klabu nyingine ndani ya ligi kuu ya Ufaransa tofauti na klabu yake ya sasa ya Angers.
Olympique de Marseille wanaelezwa kutoa kiasi cha Euro milioni 10 ili kunasa saini ya mchezaji huyo mwenye ufundi wa hali ya juu, Taarifa kutoka Ufaransa zinaeleza dili hilo lipo katika hatua za mwisho kabisa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco.
Azzedine Ounahi mpaka sasa amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya Olympique de Marseille huku mazungumzo ya mwisho yanaendelea baina ya klabu ya Olympique de Marseille na klabu ya Angers. Kuanzia leo Marseille wanaweza kumtangaza kiungo huyo kama mchezaji wao mpya.

