Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefunguka juu ya mshambuliaji wake kinara Earling Haaland kua nahodha baada ya mshambuliaji huyo kuvaa kitambaa cha unahodha jana kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle.
Wengi walionekana kuhoji juu ya Haaland kuvaa kitambaa cha unahodha siku ya jana kwani hakuwahi kuonekana kua chaguo la manahodha kwenye kikosi cha City jambo ambalo limefanya kocha Guardiola kutoa ufafanuzi juu ya hilo “Nilipiga kura kwa Erling Haaland kuwa sehemu ya kundi la manahodha.””Atakuwa hapa kwa miaka 10 na atakuwa miongoni mwa manahodha, ni sehemu ya mchakato.”
Manahodha wa klabu ya Manchester City ambao wanafahamika ni Kevin De Bruyne, Kylie Walker ambaye yupo kwa mkopo Ac Milan, na Ruben Dias hivo jana wachezaji wote hao hawakuanza kwenye mchezo dhidi ya Newcastle, na Kupelekea Haaland kuvaa kitambaa cha unahodha hii ikionesha wazi mshambuliaji huyo anaandaliwa kua nahodha ndani ya klabu hiyo.
Kutokana na kauli ya kocha Pep Guardiola ni wazi Haaland atakua nahodha wa timu hiyo kwa muda mrefu kwani ukitazama manahodha wengine wa timu hiyo ni wazi hawana muda mrefu ndani ya klabu hiyo, Hivo hii inaonesha fursa ya mshambuliaji huyo kuchukua kitambaa na kuongoza jahazi iko wazi zaidi.