Manchester United Vs Spurs Battle ya Vibonde

Kutoka kua mchezo wenye mvuto na ushindani mkubwa mpaka sasa umegeuka kua mchezo ambao unazikutanisha timu zilizopo kwenye nafasi za chini kwenye msimu wa ligi kuu ya Uingereza ni Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Tottenham Hostpurs leo watakua nyumbani kuikaribisha Manchester United ambayo tayari wameshafanikiwa kuifunga mara mbili msimu huu wakiifunga kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kwenye dimba la Old Trafford, Lakini pia wakifanikiwa kuwatupa nje mashteni hao wekundu kwenye michuano ya Carabao Cup.

Mchezo wa leo unakutanisha vibonde kwani timu inayoshika nafasi ya 15 na 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza Spurs wakiwa wa 15 Man United wao wakiwa nafasi ya 14, Ambapo leo Spurs wakifanikiwa kushinda wataishusha United mpaka nafasi ya 15.

Klabu ya Manchester United inakwenda kwenye mchezo huu ikiwa imepata taarifa za mshtuko kwani jana imetoka taarifa ya kukosekana kwa kiungo Kobbie Mainoo, Manuel Ugarte, pamoja na Amad Diallo ambaye anatarajiwa kukaa nje msimu mzima uliobaki hivo ni wazi ni mchezo ambao unatarajiwa kua mgumu kwao.

Klabu ya Tottenham wao kupitia kocha wao Ange alitoa taarifa kua anatarajiwa wachezaji wake kama golikipa namba moja Vicario, James Maddison, pamoja na beki Destiny Udogie kurejea leo dhidi ya Man United, Hii inaonesha kwa kiasi gani kikosi cha Ruben Amorim kipo kwenye wakati mgumu kwani wakati wenzao wachezaji muhimu wanarejea wa kwao wanapata majeraha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.