Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ameweka wazi kuwa hatamzuia kiungo wake nyota Rodri iwapo ataamua kuondoka na kujiunga na Real Madrid. Kauli hiyo imekuja wakati tetesi za mchezaji huyo kurejea Hispania zikizidi kupamba moto.

Guardiola amekiri wazi kuwa mvuto wa Real Madrid ni mkubwa kwa mchezaji yeyote duniani, hasa kwa Rodri ambaye ni Mhispania. Amesisitiza kuwa ni jambo la kawaida kwa mchezaji kuvutiwa na klabu kubwa kama hiyo, na anaelewa kabisa hisia hizo.
Kocha huyo ameweka msimamo wake kuwa hana nia ya kumlazimisha mchezaji kubaki kama hana furaha. Kwa mujibu wake, mchezaji yeyote ambaye anahisi muda wake umefika kuondoka, anapaswa kupewa uhuru huo bila kuzuiwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, Guardiola hakuficha umuhimu wa Rodri ndani ya kikosi chake, akimtaja kama moyo wa timu na mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani kwa sasa. Ameeleza kuwa angependa aendelee kubaki Etihad kwa muda mrefu zaidi.

Kwa sasa, Rodri bado ana majukumu makubwa na City, huku timu ikiwa kwenye mbio za ubingwa na michuano mingine mikubwa. Hatma yake itaamuliwa baada ya msimu, lakini wazi ni kwamba mlango wa Real Madrid uko wazi na Guardiola hatasimama njiani.

